MASOMO NURU YA SIKU ZA USONI


“Schulen fur Kenya” ilianzishwa mnamo mwaka wa 2005 kama kikundi ambacho hakizingatii faida bali kinaweka lengo kuu la kuendeleza masomo ya shule kwa jumla katika eneo la Ndumberi lililoko Kenya.

 

Juhudi zote za kikundi chetu zimewekwa katika mikakati dhabiti inayolenga ustawishaji wa maendeleo katika mataifa yanayojiendeleza kimaendeleo yaweza tu kuafikiwa kupitia masomo na mafunzo ya ubahili kwa vijana.

 

Tunajivunia kuwa hatutumii fedha zozote dhidi ya shughuli zetu za afisi kuu mpaka wa sasa. Fedha za matumizi hayo yanashughulikiwa na washikadau wenyewe na ambao wanajitolea kwa moyo mkunjufu.

 

Lengo letu kuu kwa sasa ni ujenzi na upanuzi wa shule ya upili ya DON BOSCO ambapo wasichana mia moja ishirini katika madarasa manne tofauti kuanzia mwaka wa tisa hadi wa kumi na mbili kujitayarisha kwa ajili ya mtihani wa mwisho. Mtihani huu ni mahitaji muhimu ya chuo kikuu na mafunzo ya ubahili katika siku zijazo.

 

Tangu mwaka wa 2013 tunafurahia kusaidia wanafunzi wasiojiweza kupitia ufadhili wetu.